Shule ya msingi Gongoni
iliyopo manispaa ya Tabora bado inaendelea kujifunzia na kufundishia
vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA kwa njia ya nadharia.
Kauli hiyo imetolewa leo na mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Gongoni bwana Khamisi Kibango wakati akizungumza na VOT FM STEREO ofisini
kwake.
Amesema kuwa hivi karibuni serikali iliahidi kuleta
vifaa vya kujifunzia na kufundishia vya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA mashuleni ili kuongeza kiwango cha ufahamu
na ufaulu kwa wanafunzi.
Mwalimu Kibango amefafanua kuwa tangu serikali
ilipoahidi kuleta vifaa hivyo utekelezaji bado haujafanyika mashuleni hali
inayowalazimu walimu kuendelea kufundisha kwa nadharia.
Aidha ameitaka serikali kupitia wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi imeombwa kutimiza ahadi iliyotoa ya kuleta vifaa vya
kujifunzia na kufundishia vya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA
mashuleni.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !