Dj Faster 80 Updates:
Home » , » Vijiji 28 vya mikoa ya Tabora na Katavi kunufaika na misitu ya miombo

Vijiji 28 vya mikoa ya Tabora na Katavi kunufaika na misitu ya miombo

Written By Voice of Tabora Radio on Tuesday, May 21, 2013 | 9:58 AM




Jumla ya vijiji 28 kutoka wilaya za Urambo, Sikonge, Kaliua, Uyui na wilaya ya Mlele mkoani Katavi vinatarajiwa kunufaika na mradi wa usimamizi endelevu wa misitu ya miombo kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizindua mradi huo uliofadhiliwa na UNDP na GEF mkuu wa mkoa wa Tabora bibi Fatuma Mwassa amewataka walengwa wa mradi kushiriki kikamilifu katika hatua zote za utekelezaji ili  kuweza kufikia malengo yaliyopo.

Amesema mradi huo utawawezesha wananchi wa vijiji husika na vijiji jirani pamoja na msitu huo kunufaika na mazao ya timbao na yale yasiyo ya timbao.

Aidha amefafanua kuwa zaidi ya dola milioni 3 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 5 zimetolewa na wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwenye kata za Mbola - wilaya ya Uyui, Imalamakoye- wilayani Urambo, Usinge - wilaya ya Kaliua, kata ya Inyonga - wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Mkuu huyo wa mkoa amesema mradi huo utasimamiwa na ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira) na katika utekelezaji utapata msaada wa kitaalamu kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.


Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii