Serikali imesema inaanza kuyapitia
upya madaraja ya zao la tumbaku ili kumnufaisha mkulima wa zao hilo.
Kauli hiyo ya serikali imefutia
swali lililoulizwa leo Bungeni mjini Dodoma na mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini
mheshimiwa Shaffin Sumar ambaye alitaka kujua ni lini serikali itayapunguza
madaraja ya zao hilo yaliyopo sasa ambayo yanamnyonya mkulima.
Akitoa kauli ya serikali naibu
waziri wa kilimo chakula na ushirika mheshimia Adam Malima amesema serikali
kupitia bodi ya tumbaku TTB wameanza kuyapitia upya madaraja hayo zaidi ya
sabini ili kuyashusha kufikia madaraja hamsini.
Katika swali lake la nyongeza
mheshimiwa Sumar alisema madaraja ya tumbaku yanayotumika tanzania ni mengi
ukilinganisha na nchi za Zambia na Zimbabwe na kwamba hayana tija kwa kuwa
yanachangia kumnyonya mkulima wa zao hilo.
Aidha mbunge huyo ameitaka serikali
kuchukua hatua dhidi ya ubadhilifu wa fedha za wakulima uliofanywa baina ya
chama kikuu cha wakulima wa tumbaku kanda ya Magharibi WETCU na mabenki kupitia
mikopo ya pembejeo na ujenzi wa maghala hali iliyosababisha wakulima kubebeshwa
madeni wasiyostahili.
Akijibu hoja hiyo naibu waziri
malima amebainisha kuwa serikali imeunda tume inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Tabora
bibi Fatuma Mwasa kushughulikia na kwamba mapendekezo yatakayotolewa
yatafanyiwa kazi na serikali.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !