Viongozi wa serikali za vijiji na kata wilayani Uyui
wameshauriwa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kuwahudumia watu wenye
ulemavu kama watu wengine.
Ushauri huo umetolewa na mbunge wa Tabora kaskazini
mheshimiwa Shafin Sumar wakati akizungumza na VOT FM STEREO kwa njia ya simu
kutoka bungeni mjini Dodoma.
Amesema viongozi hao wakizingatia misingi ya utawala
bora katika kutekeleza majukumu yao wataondoa changamoto zinazowakabili watu
wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika vikao vya maamuzi.
Mheshimiwa Sumar amebanisha kuwa endapo watu wenye
ulemavu watashirikishwa kikamilifu katika vikao hivyo watapata fursa ya
kuzisemea changamoto walizonazo na kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
Aidha amewataka watu wenye ulemavu wilayani humo
kujiamini na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi
ujao wa serikali za mitaa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuingia kwenye vikao
vya maamuzi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !