Viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu wilayani Uyui
wameaswa kuongoza kwa kuzingatia uwazi
na uwajibikaji ili kuepusha migogoro inayochangia kudhoofisha vyama hivyo.
Rai hiyo imetolewa
na mbunge wa jimbo la Tabora kaskazini mheshimiwa Shaffin Mamlo Sumar katika
hotuba yake iliyosomwa na katibu wake bwana Said Katala wakati wa ufunguzi wa mkutano
mkuu wa uchaguzi wa chama cha watu wenye ulemavu CHAWATA wilaya ya Uyui uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha
wanafunzi mjini hapa.
Mheshimiwa Shafin amesema viongozi hao wanapaswa kuwa
chachu ya mabadiliko chanya kwa kuwaunganisha wanachama wao na kuzitumia
rasilimali zilizopo kwa manufaa ya wote.
Aidha katika uchaguzi huo bwana John Kuka ametetea
nafasi yake ya uenyekiti baada ya kushinda kwa kura saba dhidi ya mpinzani wake
bwana Maganga Msabila aliyepata kura sita.
Viongozi wengine ni bwana Maganga Msabila amekuwa makamu
mwenyekiti, bwana Husseni Gea amechaguliwa kuwa katibu na bibi Hindu Lupembelo
amechaguliwa kuwa mtunza hazina wa chama hicho.
Mkutano huo umewachagua bwana Andrea Dotto kuwa naibu
katibu na bwana Ally Said kuwa mtunza hazina msaidizi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !