Serikali mkoani Tabora imewataka wakulima za zao la
tumbaku kuuza tumbaku yao kwenye vyama vyao vya msingi badala ya kuitorosha .
Mkuu wa mkoa wa Tabora bibi Fatuma Mwasa ametoa agizo
hilo leo jioni wakati akikagua maandalizi ya soko la zao hilo litakalofanyika
kesho katika ghala la kampuni ya TLTC lililopo Kiloleni mjini Tabora.
Amewataka wakulima wa zao hilo kuondoa hofu juu ya
madeni wanayodaiwa kwani hakuna mkulima atakaye katwa fedha zake kabla ya
madeni yake kuhakikiwa.
Bibi Fatuma amewaasa wakulima hao wa tumbaku kuuza
tumbaku yao kwenye vyama vyao vya msingi ili kulinda haki zao kama wanachama wa
vyama hivyo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !