Shirika la mfuko wa Bima ya afya limeanza kutoa elimu
kwa wanachama wake katika Manispaa ya Tabora ili kuwapa uelewa wa kutambua
wajibu wao katika chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu meneja wa mfuko huo
bwana Godbless Mafole wakati wa
mahojiano na VOT FM STEREO kuhusu utoaji
wa elimu kwa wanachama wao.
Amesema kuwa elimu hiyo itawasaidia wanachama kuwa na
uelewa, kujua umuhimu na kutambua wajibu wao wanapoenda hospitali kupata
matibabu.
Bwana Mafole ameelekeza kwamba wanachama wapokosa dawa
hospitali wanatakiwa kwenda kwenye maduka ya famasi wakiwa na fomu za hospitali
wanayopatia matibabu kwa ajili ya kupata dawa.
Meneja huyo
amebainisha kuwa mfuko wa bima ya afya umesajili maduka manne katika mkoa wa Tabora
pia unaendelea kusajili hadi vijijini ili kukidhi mahitaji ya dawa kwa
wanachama wao.
Aidha bwana Mafole ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Tabora
kuwa kwa yeyote mwenye uwezo wa kufungua duka la dawa lenye viwango vinavyokubaliwa watalisajili na mfuko huo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !