Waumini wa dini ya kiislam mkoani Tabora wameshauriwa
kuchukua mikopo kwenye SACCOS za kiislamu kwa lengo maalum ili kujiinua
kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
ushauri huo umetolewa na mratibu wa SACCOS ya kiislamu mkoa wa
Tabora Sheikh Said Mtungakoa wakati akizungumza na VOT FM STEREO ofisini kwake.
Ametahadharisha
kuwa baadhi ya waumini wa dini hiyo wamekuwa wakichukua mikopo
pasipokuwa na malengo maalum na mwisho wanajikuta wanatumia fedha
walizokopeshwa kwa matumizi mengine na kushindwa kufanya marejesho.
Mratibu huyo amefafanua kuwa unapohitaji kuwa mwanachama
na kuchukua mkopo ni muhimu kujipanga kwa shughuli utakayofanya ili fedha
utakayokopeshwa ijizalishe na kupata faida.
Aidha, Sheikh Mtungakoa amewataka waislam kuacha tabia
ya manung’uniko ya kuwa wao hawawezeshwi kiuchumi na badala yake amewasihi
wajiunge katika SACCOS za kiislam zisizokuwa na riba ili kujiendeleza na
hatimae kujiinua kiuchumi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !