Picha kwa Hisani ya Mtandano-Maktaba |
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imepokea shilingi millioni
600 hadi sasa kutoka mfuko wa
barabara kwa ajili ya ujenzi wa barabara
ikiwa jumla ya fedha zilizotengwa ni zaidi ya shilingi billioni moja nukta moja.
Kauli hiyo imetolewa na mhandisi wa ujenzi wa barabara Manispaa ya
Tabora bwana Edward Lemelo wakati wa mahojiano maalumu na VOT FM STEREO kuhusu
utekelezaji wa ujenzi wa barabara za Manispaa hiyo.
Amezitaja barabara ambazo zimekamilika hadi sasa kuwa ni
barabara ya Kisarika yenye urefu wa kilometa 24 nukta 46, barabara ya Soweto
yenye kilometa 0.67, barabara ya Mwinyi
yenye kilometa 2 nukta 1 na barabara Ndevelwa yenye urefu wa kilometa 19 nukta 85.
Amesema ujenzi wa barabara ulianza mwaka jana
ukiwa umegawanyika katika makundi makuu mawili ya matengezo ya kawaida na matengenezo makubwa
unaotarajiwa kumalizika Juni 30 mwaka huu.
Aidha bwana Edward amesema halmashauri ya Manispaa ya
Tabora katika mwaka huu wa fedha imetenga fedha kwa ajili ya kuweka lami
barabara ya Lumaliza - Mwanza yenye kilometa
mbili ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka.
Mhandisi huyo amebainisha kuwa wamekarabati greda la
kuchonga barabara ambazo hazipo kwenye orodha na zoezi hilo litaanza muda
wowote kwa kila kata.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !