Dj Faster 80 Updates:
Home » , » Mtu mmoja ajeruhiwa kwa risasi na kuporwa fedha taslimu

Mtu mmoja ajeruhiwa kwa risasi na kuporwa fedha taslimu

Written By Voice of Tabora Radio on Wednesday, May 29, 2013 | 7:49 PM



Mkazi mmoja wa maeneo ya Upuge wilaya ya Uyui mkoani Tabora ameporwa fedha na watu wasiojulikana na kisha kupigwa risasi miguuni.

Kamanda wa polisi mkoani Tabora bwana Peter Ouma amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu usiku.

Amemtaja mtu huyo aliyeporwa fedha kuwa ni bwana Hasani Saidi mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa wilayani humo.

Kamanda ouma amesema watu hao wasiofahamika walivamia nyumbani kwa bwana Saidi na kumnyang’anya fedha ambazo hazijafahamika kiasi chake  na kisha kumpiga risasi miguuni na amelezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoani Tabora Kitete.

Aidha katika tukio hilo hakuna mtu aliyekamatwa na jeshi la polisi mkoani Tabora linaendelea na upelelezi wa kuwabaini wahusika ili waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii