Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Tabora
wameshauriwa kuwa na ushirikiano katika kuhamasisha waumini wao kuhusu
uchangiaji damu.
Ushauri huo umetolewa leo na afisa mhamasishaji wa Mpango
wa taifa wa damu salama kanda ya Magharibi bwana Costantine Thadeo wakati
akizungumza na VOT FM STEREO.
Amesema kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwahamasisha
waumini kuhusu uchangiaji damu ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea kupitia
mpango huo wa taifa wa damu salama.
Afisa huyo wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya Magharibi
amesema katika kipindi cha maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu kwa mwaka huu
wanatarajia kukusanya chupa zaidi ya
1,500.
Bwana Thadeo amefafanua kuwa malengo mengine
waliojiwekea ni pamoja na kuendelea kuhamasisha jamii kuchangia damu, kutoa
elimu kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na kwa jamii kupitia vyombo
vya habari na mikutano ya hadhara.
Aidha maadhimisho hayo ya uchangiaji damu duniani
hufanyika juni 14 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika mkoani
mara na kwamba yamebeba ujumbe wa kauli mbiu isemayo changia damu ni zawadi ya
maisha.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !