Asilimia 40 ya wauguzi wanahitajika katika kata
za manispaa ya Tabora ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye vituo vya
afya.
Kauli hiyo imetolewa na afisa muuguzi wa manispaa ya
Tabora bibi Devota Msele wakati akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uwajibikaji.
Amesema wauguzi hao wanaohitajika ni kwa ajili ya vituo
vya afya wilayani Tabora ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wakati wa
kutibiwa.
Bibi Devota ameitaja changamoto nyingine kuwa ni
upungufu wa vifaa tiba zikiwemo dawa hali ambayo huwalazimu baadhi ya wagonjwa
kununua dawa walizoandikiwa kwenye maduka ambazo hazipo hospitali.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !