Dj Faster 80 Updates:
Home » , » Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi

Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi

Written By Voice of Tabora Radio on Wednesday, May 22, 2013 | 1:12 PM



Jeshi la polisi mkoani Tabora limewakamata watu wanne wakazi wa wilayani Nzega kwa tuhuma za kuingia eneo la mgodini kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi mkoani Tabora bwana Peter Ouma amesema kuwa watu hao walikamatwa baada ya kuingia kwenye mgodi wa Lusu pasipo kuwa na kibali maalum.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Juma James mwenye umri wa miaka 23, Masanja Shija mwenye umri wa miaka 26, Lucas Masanja mwenye miaka 21 pamoja na Maige Sangu mwenye umri wa miaka 28.

Kamanda Ouma amefafanua kuwa baada ya kukamatwa walihojiwa na jeshi la polisi na walikosa kutoa majibu yaliyo sahihi na kwamba jeshi hilo linadhani walikuwa na ni ambaya ndani ya mgodi huo.

Aidha ameitaka jamii kufuata utaratibu na sheria za sehemu husika ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii