Dj Faster 80 Updates:
Home » , » Rage aishauri serikali kuongeza watumishi shirika la reli

Rage aishauri serikali kuongeza watumishi shirika la reli

Written By Voice of Tabora Radio on Tuesday, May 21, 2013 | 9:40 AM

Reli | Picha-Mtandao


Mbunge wa Tabora mjini mheshimiwa Ismail Aden Rage ameishauri serikali kuwekeza katika raslimali watu kwenye shirika la reli ili kuliongezea ufanisi wa kiutendaji.
Mheshimiwa Rage ameyasema hayo hii leo mjini Dodoma ambapo alieleza kuwa shirika hilo lina kabiliwa na upungufu wa watumishi na hivyo ingefaa kuwarudisha kazini wastaafu wenye uzoefu.

Amesema hatua hiyo itarahisisha usimamizi wa miradi mbalimbali ambayo inatarajiwa kuanzishwa na serikali hususan uboreshaji wa reli ya kati.

Aidha  mbunge huyo amebainisha kwamba Tabora kuna karakana ya reli ambayo haifanyi kazi hivyo ameiomba serikali iangalie uwezekano wa kuitumia karakana hiyo ili iweze kusaidia ukarabati wa mabehewa.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii