Serikali imesema kuwa miradi ya usambazaji wa huduma
ya umeme vijijini unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.
Waziri wa nishati na madini mheshimiwa Sospeter
Muhungo ametoa kauli hiyo Bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Busanda mheshimiwa Lolensia Bukwimba
aliyetaka kufahamu ni lini miradi hiyo ya usambazaji wa nishati ya umeme
vijijini itakamilika.
Mheshimiwa Muhongo amefafanua kuwa kulingana na
wafadhili wa miradi hiyo ambao ni serikali ya Marekani miradi hiyo inatarajiwa
kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha
utekelezaji wa miradi hiyo ndani yake kuna miradi midogo arobaini na moja ya
usambazaji wa umeme kwenye mikoa kumi na sita ya tanzania bara miongoni mwa
mikoa hiyo ni Tabora, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, na Tanga.
mikoa
mingine ni Pwani, Morogoro, Dodoma,
Singida, Mbeya, Rukwa, Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara pamoja na Shinyanga.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !