Dj Faster 80 Updates:
Home » , » wafanyakazi wa kampuni ya CEFTEC wakamatwa kwa kujeruhi mwenzao

wafanyakazi wa kampuni ya CEFTEC wakamatwa kwa kujeruhi mwenzao

Written By Voice of Tabora Radio on Monday, May 20, 2013 | 10:34 PM



Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Tabora kufuatia tukio la kupigwa na kujeruhiwa kwa mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Tabora - Nyahuwa  CEFTEC  bwana Alex Semindu Ijumaa iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Tabora bwana Peter Ouma amesema watu hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Bwana Alex Semindu ambaye alikuwa opareta wa mashine aina ya stebolizer kwenye kampuni ya CEFTEC, alipigwa na kujeruhiwa vibaya na walinzi wa kampuni hiyo huku wakishirikiana na wasimamizi wawili wa kichina na kupelekea kulazwa katika hospitali ya mkoa Kitete.  

Akizungumza hospitalini hapo bwana Alex Semindu amesema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya kuchoshwa na dharau za wasimamizi wake hivyo kuamua kuacha kazi na kudai fedha zake kitu ambacho hakikukubaliwa na wasimamizi hao.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii