Dj Faster 80 Updates:
Home » , » Jeshi la polisi mkoani Tabora lawashikilia watu wawili kwa kukutwa na bangi

Jeshi la polisi mkoani Tabora lawashikilia watu wawili kwa kukutwa na bangi

Written By Voice of Tabora Radio on Monday, May 20, 2013 | 10:31 PM



Jeshi la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wawili wakazi wa mjini Tabora kwa tuhuma za kukutwa na kete 38 za bangi.

kamanda wa polisi mkoani tabora bwana Peter Ouma amesema kuwa watu hao wamekamatwa Mei 18 mwaka huu kufuatia msako unaoendelea mkoani Tabora.

Bwana Ouma amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa na kete hizo za bangi kuwa ni Hamisi mbao mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora ambaye alikutwa na kete sita. 

Aidha mtu mwingine  aliyekutwa na kete 32 za bangi  ni Ramadhani Hamisi mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kata ya Ng’ambo mjini hapa.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora amebainisha kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Listen Live VOT FM.High quality

Total Visit


TELECENTRE

Michezo Videos

 
Powered by Blogger | © Voice of Tabora Radio 89.0Mhz - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii